Hiltan Kalugho alitoweka nyumbani kwake mwaka 1980 na kupotelea katika taifa jirani la Tanzania akisaka njia ya kuboresha maisha ya familia yake
Hata hivyo, alisema alishindwa kurudi nyumbani sababu alikosa kupata pesa alizokuwa natarajia kupata kukithi mahitaji ya familia yake
Wakati aliporejea nyumbani kwake wiki jana, mzee huyo alishtuka kupata mkewe pamoja na wanawe wawili wa kiume walikuwa wamefariki dunia
Mzee mwenye umri wa miaka 94, ambaye aliondoka nyumbani kwake katika kijiji cha Majengo, kaunti ya Taita Taveta, miaka 42 iliyopita, ameungana tena na familia yake.
Mwenda tezi: Mzee Arejea Nyumbani kwake Baada ya Miaka na Kupata Mkewe Amefariki
Mzee Hiltan Kalugho(kwenye upande wa kulia) alitoweka nyumbani kwake mwaka 1980 na kupotelea katika taifa jirani la Tanzania. Picha: Nation. Source: UGC
Hiltan Kalugho alitoweka nyumbani kwake mwaka 1980 na kupotelea katika taifa jirani la Tanzania akisaka njia ya kuboresha maisha ya familia yake.
Hatua ya Kalugho iliwacha familia yake na dhiki, akiwacha nyuma mke na watoto saba, huku juhudi zao za miaka mingi kumsaka zikikosa kuzaa matunda.
Wakati aliporejea nyumbani kwake wiki jana, mzee huyo alishtuka kupata mkewe pamoja na wanawe wawili wa kiume walikuwa wamefariki dunia.
Read also
Stanley Livondo Awasha Joto la Kisiasa na Madai Kulikuwa na Njama ya Kumuua Rais Uhuru
Akizungumza na Nation, alisema alikuwa na matumaini ya kukutana tena na mke wake Dreda Mshai, ambaye aliaga dunia mwaka 2007 akiwa na umri wa miaka 75 pamoja na wanawe wote.
"Najisikia vibaya sana kwamba baadhi ya wanafamilia yangu hawapo hapa kushuhudia muungano huu. Nilitamani sana kumuona mke wangu na watoto wangu wote," alisema Kalugho.
Katika mahojiano na gazeti hilo, mkongwe huyo alisema alifunga safari ya kuelekea Tanzania kuwatafutia watoto wake maisha mema.
Hata hivyo, alisema alishindwa kurudi nyumbani sababu alikosa kupata pesa alizokuwa natarajia kupata kukithi mahitaji ya familia yake.
Kalugho pamoja na marafiki zake waliishi katika kijiji cha Mororoni nchini humo ambako alifanya kazi katika migodi ya madini ya vito.
“Tulikuwa tunapata mawe hayo na kuyauza. Sisi, hata hivyo, hatukupata mafanikio yoyote. Tulichokuwa tukipata kilitosha tu kututegemeza," aliongeza.
Kisha, alistiriwa na familia moja ambayo alikuwa akiwachungia mifugo yao.
Kwa miaka yote hiyo, alisema kuwa hakuwahi kuoa tena kwani alikuwa na matumaini siku moja angewaona watoto wake nchini Kenya