Mzunguko wa pili Ligi kuu Tanzania bara kuanza leo

 


Mzunguko wa pili wa ligi kuu soks Tanzania bara unaanza rasmi jioni ya leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika dimba la Nyankumbu mkoani Geita ambapo the pride of geita, Geita gold FC watawakaribisha wauwaji wa kusini Namungo fc kutoka Ruangwa mkoani Lindi.


Ikumbukwe mzunguko wa kwanza ulikamilika huku klabu yanga ikiwa ndio timu iliyofunga magoli mengi zaidi ikiwa imefunga jumla ya magoli 25 na pia ndio timu iliyofungwa magoli machache magoli zaidi, ikiwa imefungwa magoli manne pekee.


Na mahasimu wao klabu ya Simba ikiongoza kwa timu zilizoshinda michezo mingi ya uwanja wa nyumbani, ikiwa imeshinda michezo 6 kati ya michezo 8, na Yanga ikiwa timu iliyoshinda michezo mingi ugenini ikishinda michezo 7 kati ya michezo 9. Na klabu ya Ruvu shooting ikiwa ndio timu ilyofungwa magoli mengi zaidi ikifungwa jumla ya magoli 21 katika michezo 15.


Ligi hiyo itaendela kesho kwa michezo miwili ambapo mbeya kwanza watawakaribisha wakata miwa wa Mtibwa Sugar katika Dimba la Sokine jijini Mbeya majira ya saa kumi jioni, huku watoto wa kinondoni klabu ya KMC ikiminyana na maafande wa polisi Tanzania majira ya saa 1 usiku katika dimba la Azam Comlpex Chamazi jijini Dar es salaam.


Na Michezo ya jumapili ni Ruvu shooting dhidi ya Dodoma jiji saa 8 mchana, Tanzanaia Prisons dhidi ya Mbeya City saa 10 jioni, na Yanga dhidi ya Kagera sugar saa 1 usiku

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad