WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amempongeza Rostam Aziz kwa kuwalipa stahiki za mafao kupitia mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PSSF na NSSF waliokuwa Wafanyakazi wa New Habari (2006) Ltd.
Nape alitoa pongezi hizo baada ya wafanyakazi hao kupokea hundi ya Sh Bilion 2.9 kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni hiyo, Lyakurwa ambapo kiasi hicho cha hundi kitawekwa katika mifuko hiyo.
Sanjari na pongezi hizo Nape amewakumbusha waajiri wote kuwalipa mishahara watumishi katika idara mbalimbali, kuwapa mikataba ya ajira kwa mujibu wa sheria na kupeleka mafao yao katika mifuko ya hifadhi ya Jamii nchini.
Nape aliitaka mifuko yote miwili kuharakisha ulipwaji wa mafao hayo ili kila mmoja apate haki yake kwa mujibu wa sheria na kwamba siku zote serikali itaendelea kusimamia maslahi ya waandishi wa habari.