Waziri wa Habari Nape Nnauye, amesema kuwa wamefanya mabadiliko na kwamba chaneli za bure kama ITV na East Africa TV zimeanza kuonekana tena kwenye king'amuzi cha DStv baada ya hapo awali kuondolewa.
Taarifa hiyo ameitoa hii leo Januari 31, 2022, na kusema kuwa mabadiliko yaliyofanyika ni ya kanuni namba 18 ya mwaka 2018, na kusema kuwa Rais Samia amemwagiza kufanya mabadiliko na kanuni zimeshasainiwa na tayari zimeanza kutumika ili kuongeza wigo kwa Watanzania kupata habari.
"Tumefanya mabadiliko, chaneli ambazo hazilipiwi zianze kuonekana kwenye king'amuzi cha DStv, mtakumbuka baadhi ya chaneli ziliondolewa kwenye king'amuzi chenu na hili jambo limekuwa kilio kikubwa kwa wananchi, Rais kaniagiza na nimefanya mabadili," amesema Waziri Nape