Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Serikali inaendelea kuchambua malalamiko ya matumizi ya 'Bundle' kwenye simu
Amefafanua, "Malalamiko kwamba kuna 'Bundle' zinawekwa kwenye Simu, zinatumika bila Mtumiaji kuzitumia yamekuwepo, yamefikishwa Mamlaka husika na Uchambuzi umefanyika. Matokeo yanaonesha hakuna wizi uliotokea, isipokuwa kuna tatizo la matumizi ya simu za kisasa"
Ameongeza, "Matatizo hayo yamejikita kwenye maeneo mawili; 1) Hizi simu za kisasa wakati mwingine hata ukiwa hutumii, kuna baadhi ya 'Applications' zinaendelea kufanya kazi nyuma ya simu. 2) Simu hizi unaweza kuweka 'Bundle' lako ukawasha 'Hotspot' ambayo inaruhusu mtu mwingine kutumia Data uliyonayo"