Ninahisi tumefanyiwa uchawi, kipa wa Man United David De Gea adai



Kipa David De Gea sasa anadai kuwa klabu yake ya Mancheseter United huenda imerogwa
Man United imekuwa katika mahangaiko tangu kocha matata Sir Alex Ferguson kustaafu mwaka 2013 na mara ya mwisho kushinda taji lolote ni 2017
Klabu hiyo ilitarajiwa kupigania taji la EPL msimu huu lakini sasa hata kumaliza katika bano la nne bora inaonekana kuwa mtihani mgumu
Mlinda lango David De Gea sasa anadai kuwa huenda Manchester United ililaaniwa, klabu hiyo inapoendelea kupitia mahangaiko msimu huu.

Kipa wa Man United David De Gea Adai Klabu hiyo Huenda Imerogwa
Kipa wa Manchester United David De Gea baada ya kupigwa bao katika mechi iliyopita.
Ndoto ya Man United kuokoa msimu wao huenda isitimie klabu hiyo sasa ikipeleka nguvu zake kujihakikishia nafasi ya nne bora katika Ligi Kuu ya Uingereza, lakini hilo pia kwa sasa linaonekana kuwa mtihani mgumu.

Klabu hiyo ilianza msimu ikiwa na matumaini ya kupigania taji la EPL, lakini imedhihirika wazi kuwa United huenda wakamaliza msimu mwingine bila kushinda taji lolote na De Gea anasema huenda wamerogwa.

“Ninadhani mtu alituroga. Ukweli ni kwamba sielewe kinachoendelea, sielewi kabisa,” De Gea alisema katika mahojiano na gazeti moja la Uhispania la El Pais.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad