Nuh Mziwanda Amemuomba Radhi Mume wa Shilole "Naheshimu Ndoa yenu"




Hii leo kwenye Empire ya EFM,Akijibu swali la mtangazaji B Dozen, kama anahisi kuachana kwake na @officialshilole kumempunguzia mashabiki, @iam_mziwanda amejibu hapana, maana anaamini mashabiki zake wamempendea muziki anao ufanya na si kwasababu alikuwa kwenye mahusiano na Shilole.

Akijibu pia swali la Dozen kuwa haoni kama anacho kifanya hivi sasa kuhusu Shilole kina hatarisha ndoa ya Shishi na kumkosea Rommy ambaye ni mume wa Shishi,huku akitaka avivae viatu vya Rommy kwa sasa, Nuh Mziwanda amemuomba Radhi, @rommy3d kama atakuwa anakerekwa na kile anacho kiongea kuhusu mkewe, lakini atambue anacho kiongea haongei kwa Lengo baya la kutaka wao wagombane au ndoa yao ivunjike, bali anaongea kwa kuwa ni hisia zilizo baki moyoni mwake,akikazia kwa kusema anaiheshimu ndoa ya Shilole na anaipenda pia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad