Pablo Aunga Mkono Morrison Kusimamishwa Simba




Pablo aunga mkono Morrison kusimamishwa Simba
KOCHA mkuu wa Simba Pablo Franco ameunga mkono hatua ya Mtandaji Mkuu wa timu hiyo Barbara Gonzalez kumsimamisha kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison.

Akizungumza na Spotileo kocha huyo amesema pamoja na kutambua kipaji alichonacho Morrison, lakini mchezaji huyo ni tatizo ndani ya timu na mara nyingi amekuwa akishindwa kutimiza maelekezo anayoyatoa hata wanapokuwa mazoezini.

"Ni maamuzi sahihi ambayo mtendaji mkuu ameyachukua kwa ajili ya faida ya timu maana kukaa na mchezaji asiyefuata maelekezo ya kambi ni sawa na kuishi na msaliti muda wowote anaweza kutoa siri zenu kwa mpinzani hicho ni kitu kibaya kwenye mpira hasa ukizingatia tunapita katika kipindi kigumu," amesema Pablo.

Kocha huyo amesema anaamini hilo litakuwa funzo hata kwa wachezaji wengine ambao walikuwa wakiwaza kufanya utovu wa nidhamu kama ilivyokuwa kwa Morrison.


Bernard Morrison mwanasoka wa kimataifa raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 29 alijiunga na Simba 2020 akitokea Yanga.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad