Comfort Akosua Nyarkoa na Grace Akosua Nyarkoa, 87, wanasemekana kuwa pacha wenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuishi kwa muda mrefu katika eneo la Akwamufie mashariki mwa Ghana.
Akwamufie ni jimbo na makao makuu ya jimbo au ufalme wa Akwamu ambapo Chifu Mkuu, Odeneho Kwafo-Akoto III, na Malkia Nana Afrakoma II wanaishi na kuendesha shughuli zao.
Licha ya umri wao wa miaka 87, wakongwe hao bado wana nguvu ya kujishughulisha na shughuli nyingi bila msaada wowote kwa mujibu wa Wikipedia na Ajuza hao wameishi kwa miongo mingi na kushuhudia Ghana ikipata uhuru mnamo Machi 6, 1957.
Wawili wamejipatia umaarufu mtandaoni baada ya mshawishi wa mitandao ya kijamii wa Ghana Nänä Teä, ambaye jina lake kamili ni James Annor Tetteh kupakia picha zao akisherekea pamoja nao siku yao ya kuzaliwa. Akipakia picha hizo Nänä Teä aliandika: ”Jana ikiwa ni siku yangu ya kuzaliwa, nilinunua vitu vichache vya kupanda katika maisha yao na kuvutia aina hii ya neema (uzee katika afya njema n wasichana mapacha). Niamini, mapacha hawa wanaweza kula chochote bila matatizo yoyote ya afya. Walituombea dua kuhusu afya njema na maisha marefu na pia mapacha zaidi,” posti yake ilisoma.