PAULA Kajala ni modo, video vixen na mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii ambaye ni binti wa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja na producer wa Bongo Feleva, P Funk Majani.
Kwa sasa, Paula ambaye ni mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny yupo masomoni
nchini Uturuki na anafanya hivyo ili aje kuishi maisha mazuri bila kumtegemea mtu.
Mrembo huyo amekuwa maarufu zaidi baada ya kuwa na Rayvanny akituhumiwa kuvunja uhusiano wa jamaa huyo na baby mama wake, Fahyma.
Hata hivyo, juzikati walizima tetesi za kuachana kwamba baada ya kufuatana kwa mara nyingine kwenye kurasa zao za Instagram.
Akiwa nchini Uturuki, kama kawaida yake, Paula ameendelea kuwachimba mkwara baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimuandama mitandaoni wakidai amepora mwanaume wa mtu.
Katika moja ya posti zake, Paula anasema; “Nyie hizi fashion hizi, hii yote ili nipate picha nzuri ya kitchen party, mtanikoma nikirudi...”
Paula anamaanisha kwamba, atakaporejea nchini Tanzania atakuwa na mvuto wa aina yake wa kuwafanya watu wampende zaidi.