Profesa Jay Anavyopigania Uhai Wake, Tujitoe Kuokoa Maisha Yake




ZILIKUWA ni wiki takriban mbili za mashabiki kuwa gizani na kutokujua kama ni kweli au si kweli.  Lakini sasa, familia ya gwiji wa muziki wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ imejitokeza hadharani na kuthibitisha kuwa ni kweli staa huyo ni mgonjwa na anapigania uhai wake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.

Baada ya taarifa hiyo, hatimaye baadhi ya mastaa wenzake kila mmoja kwa nafasi yake ameeleza kuguswa na namna staa huyo anavyopigania uhai wake kitandani.

Mastaa hao wametumia muda wao kwa ajili ya kumuombea ili aweze kupona haraka.

Mbali na msanii mwenzake, Ambwene Yessayah ‘AY’ ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kutoa taarifa ya michango, lakini pia mastaa wengine kama MwanaFA nao hawakubaki nyuma kwani kupitia akaunti zao za kijamii wameandika waraka mbalimbali wakimuombea mwenzao aweze kurudi haraka katika hali yake.


 
HAMIS MWINJUMA ‘MWANAFA’:

“Kaka yangu Profesa Jay anapigania maisha yake kitandani…kaka yangu ni mgonjwa…Hakuna asiyejua makubwa aliyoyafanya kwa mziki wetu. “Alitunyooshea sana njia, yeye peke yake..akatubadilishia uelekeo kabisa na muziki wetu ukakosa mipaka, si kwa rika si kwa jinsia, ukawa wa kila mmoja.

“Binafsi sina cha kumlipa kwa ‘uongozi’ wake wa moja kwa moja ama wa mbali kwangu. Nawaomba tu tuoneshe mapenzi yetu kwa kuchangia matibabu yake ambayo gharama yake ni kubwa MNO… Tujitoe kuokoa maisha ya MC bora wa muda wote nchi hii.”

ALI SALEHE KIBA ‘KING KIBA’

Naye ni miongoni mwa mastaa wakubwa waliomposti Jay katika akaunti zao za kijamii na kumuombea ambapo yeye ameandika ujumbe mfupi uliosomeka; “Get well soon my brother…”


JACQUELINE WOLPER:

“Pole kaka yetu, jamani ndugu jamaa na marafiki tuungane kuchangia na sisi wasanii pia tusiposti tu, bali tuchangie pia.”

RAJAB ABDUL ‘HARMONIZE’:

Huyu naye ameandika ujumbe uliosomeka; “Let’s do this my people, let’s show some love to the legend…”

RAYMOND MWAKYUSA ‘RAYVANNY’

Msanii mwingine ambaye alimuombea Profesa Jay ni pamoja na Rayvanny ambaye ujumbe wake unasomeka; “Quick recovery my brother…”

FAUSTINA CHARLES ‘NANDY’

Mwanadada mrembo Nandy naye ameandika: “Get well soon my brother…”


 
ZUHURA OTHMAN ‘ZUCHU’

Mrembo Zuchu naye hakubaki nyuma kwa kushirikiana na timu yake ya Wasafi walifunga safari hadi hospitalini alikolazwa Profesa Jay kwa ajili ya kumuona na ujumbe wake ni huu;

“Mimi pamoja na timu nzima ya ya Kipindi cha Good Morning cha Wasafi tulipata wasaa wa kwenda kumtembelea super woman wetu mke wa our legend brother Profesa Jay kwa ajili ya kumtakia kheri na kumjulisha kwamba tupo pamoja naye kwenye kipindi kigumu anachopitia. Lengo pia ni kumjulisha kuwa sisi na Watanzania walio wengi tuko pamoja nao na tunamuombea yeye na kaka yetu…”

Mastaa wengine walioposti picha ya lejendi huyo katika akaunti zao za mitandao ya kijamii na kumuombea heri kwa Mwenyezi Mungu ili aweze kupona haraka ni pamoja na Diamond Platnumz, Shilole, Aunt Ezekiel, Fahyma, Kajala, Billnass, Dully Sykes, Lyyn na wengine wengi.

Kama umeguswa na tatizo la Profesa Jay na ungependa kumchangia chochote ili aweze kuendelea kupatiwa matibabu, basi unaweza kuchangia chochote ulichonacho na michango yote itapokelewa na familia kwa niaba yake kupitia MPESA: 0757919192 Joseph Haule, TiGOPesa: 0715919192 Joseph Haule,

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad