RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Brigedia Jenerali, Yohana Mabongo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Brigedia Jenerali Mabongo ni MKuu wa Tehama wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
Uteuzi huo umeanza tarehe 24 Februari 2022.
Taarifa ya uteuzi huo, imetolewa leo Jumapili, tarehe 27 Febriari 2022 na Zuhura Yunus, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.