Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba wakati anamteua Joshua Nassari, kuwa mkuu wa wilaya alimtaka aende akayatekeleze yale yote aliyokuwa akiyafanya bungeni na kwamba amekuwa miongoni mwa wakuu wa wilaya waliosifia kwa kufanya vizuri.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 7, 2022, mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa miundombinu ya kusafisha na kutibu maji uliopo Bunda mkoani Mara.
"Nimewaletea wakuu wa wilaya wachanga wachanga ili waweze kwenda mbio na ninashukuru Nassari amesifiwa sana, kwa wale wasiomjua alikuwa anatuchachafya bungeni lakini aliposema nimesalimu amri naungana na nyie na mimi nikamuambia yale uliyokuwa unayasema bungeni kayatekeleze na mtihani wako wa kwanza nakupeleka Mara, nashukuru nimesikia unafanya vizuri," amesema Rais Samia