Rais Samia ashtushwa polisi kujichunguza mauaji Mtwara



RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuunda kamati ya kufanya uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoani Mtwara huku akilitaka jeshi hilo kujitafakari.

RAIS Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na wananchi leo akiwa wilayani Magu Jijini Mwanza akielekea  mkoani Mara kuhudhuria maadhimisho ya miaka 45 ya kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Samia amesema kuna mauaji yametokea Mtwara na kwa taarifa zilizopo ni Jeshi la Polisi ndilo lililofanya mauaji huku taarifa alizonazo jeshi hilo limetengeneza kamati ya kufanya uchunguzi.

Amesema haiwezekani jeshi lifanye mauaji hilo hilo lijichunguze lenyewe alafu walete taarifa hivyo amemuagiza Waziri Mkuu kuunda kamati nyingine iende ikafanye uchunguzi wa mauaji yaliyofanywa na jeshi hilo.

" Ndugu wananchi tusubiri taarifa ya tume huru itakayoundwa na Waziri Mkuu ituletee taarifa tuilinganishe na ya Jeshi la Polisi tuone taarifa hizo zinasemaje tuchukue hatua muafaka,"amesema Samia.


 
Pia aliwaomba wananchi kudumisha amani na kuacha kufanya mauaji kwa sababu yeyote.

Awali  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ameeleza kuwa walipokea fedha za kujenga vyumba vya madarasa pamoja na shule shikizi vyumba 32 ambapo kazi ilifanyaka lakini kuna watu waliiba fedha hiyo.

Amesema hawakupiga kelele baada ya jambo  hilo hivyo  kuna watu walikamatwa na wengine wapo ndani  katika Halmashauri ya Buchosa.


"Tulisema tutasema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu chenchi imebaki zaidi ya million 600 kwenye miradi yote hii tuliamua kusimamia na tutaendelea kusimamia,"amesema Mhandisi Gabriel.

Ameongeza kuwa watahakikisha fedha zote zinazokuja mkoani hapo zinakuwa salama na inatumika ipasavyo. 

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Lilipotuhumiwa Bunge kutokea uraiani, ni Bunge hilohilo ndio liliunda jopo la uchunguzi! Inaitwa, "mbwa kamata mbwa!" Auvkedi ya nyani upelekwe kuwa nyani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad