Rais Samia ameipatia Makumbusho ya Taifa nchini kiasi cha shilingi bilioni 2.4 ili iweze kutekeleza miradi 15 inayotekelezwa kwa fedha za miradi ya ustawi wa nchi na mapambano dhidi ya UVIKO-19, katika vituo vyake sita kikiwepo cha Azimio la Arusha Jijini Arusha.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho hayo Dkt Noel Lwoga, wakati wa uzinduzi wa mradi mkubwa wa maboresho ya kituo cha Makumbusho ya Azimio la Arusha na Makumbusho ya Elimu Viumbe inayotekelezwa chini ya mpango wa miradi ya ustawi wa nchi na mapambano dhidi ya UVIKO-19.