Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya ya Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini kwa matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo.
Mkuu huyo wa nchi ametangaza utenguzi wa wakurugenzi hao leo Ijumaa Februari 4, 2022 akiwa njiani Magu jijini Mwanza akielekea Musoma mkoani Mara yanapofanyika maadhimisho ya miaka 45 tangu kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Siku ile tunazitangaza fedha nilisema kama mkurugenzi anataka kuona rangi yangu halisi achezee hizo fedha, sasa kwa traarifa zilizopo, Buchosa, Iringa, Mbeya na Singida Mjini, wakurugenzi wamechezea fedha. Mheshimiwa waziri (Waziri wa Tamisemi) wakurugenzi hao nimewatengua sasa hivi” amesema Rais Samia nakuongeza
“Yule wa Geita endeleeni na uchunguzi, na mimi timu yangu iko pale inafanya uchunguzi naye wakiniletea na makossa kama haya nay eye attatenguliwa” amesema
Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa alisema kuwa Wizara hiyo ilipata taarifa za ubadhirifu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kuhusu Wilaya ya Buchosa na maeneo mengine.
Baada ya kumaliza, Rais Samia alimuagiza Bashungwa kutaja maeneo mengine ambayo kumefanyika ubadhirifu
“Hivi sasa Ofisi ya Rais Tamisemi tunafanya uchunguzi katika halmashauri ya Jiji la Mbeya, Singida, Iringa Mjini" amesema Bashungwa
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE