Rais Samia Suluhu Hassan amezungumzia mauaji yaliyotokea Mtwara ambapo Maafisa wa Jeshi la Polisi wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mfanyabiashara Mussa Hamisi
Rais amesema haiwezekani Jeshi kutuhumiwa kisha liunde Kamati ya kujichunguza lenyewe, hivyo amesema ameagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuunda Kamati nyingine kuchunguza tukio hilo
Amesema taarifa ya Kamati ya Polisi inayochunguza tukio hilo italinganishwa na taarifa ya Kamati Huru itakayoundwa na Waziri Mkuu