Rais wa Senegal Amewazawadia Wachezaji wote wa Timu ya Taifa Kila Mmoja Mamilioni Haya na Kiwanja Juu


Baada ya Timu yao ya soka kushinda kombe la Afrika kwenye AFCON 2021 weekend iliyopita, Rais wa Senegal amewazawadia Wachezaji wote wa Timu ya Taifa kila mmoja $87,000 ambayo ni sawa na Tsh. milioni 201 ambapo ukiachia pesa Wachezaji hao pia kila mmoja amezawadiwa kiwanja kwenye Mji mkuu wa Dakar na mji wa jirani uitwao Diamniadio.

Rais wa Senegal Macky Sall amesema Timu hiyo ya Taifa imelipa Taifa hilo ushindi ambao ulisubiriwa kwa miaka na miaka hivyo wanastahili Tuzo ya heshima na Wachezaji wake wanastahili zawadi ambazo daima watazikumbuka na kumsifia sana kocha wa Timu hiyo Aliou Cissé.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad