Rais wa Senegal Atangaza Jumatatu kuwa Likizo Kufuatia Ushindi wa AFCON




Senegal wanyakua taji la kwanza la Afcon kwa kuibwaga Misri
Baada ya ushindi wa Senegal dhidi ya Misri Jumapili usiku, rais wa nchi hio Macky Sall alitangaza Jumatatu kuwa siku ya likizo kusherekea ushindi wa taji lao la kwanza la Kombe la mabingwa Afrika(AFCON) .

Kupitia runinga ya taifa, Sall alitangaza kuwa safari zote alizopanga kusafiri ameahirisha hadi sherehe hizo zifikie kikomo.


Rais huyo aliye mamlakani alipaswa kuzuru nchi ya Comoros Jumatatu lakini safari yake ilikatizwa baada ya ushindi mkubwa dhidi ya Misri.

Sall alieleza kuwa alighairi nia, ili kubisha kuwa kuwakaribisha timu ya taifa watakapokuwa wakirejea nchi hio la Kombe la AFCON Jumatatu saa 12.

Senegal ilibwaga Misri kupitia matuta ya penati ambapo waishinda 4-2.


Senegal ikiongozwa na nyota wa Liverpool sadio Mane walitangazwa mabingwa wa AFCON 2021 kwenye fainali ya kuvutia macho nchini Cameroon.

Ikumbukwe Senegal wameshindwa mara mbili katika fainali za awali mwaka wa 2002 na 2019 mtawalia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad