Volodymyr Oleksandrovych Zelensky alizaliwa 25 January 1978, ni mwanasiasa, mwandishi wa filamu, mwigizaji wa filamu, mchekeshaji na Rais wa sasa (wa 6) wa Ukraine toka 20 Mei 2019.
Kabla ya kujihusisha na siasa, alipata shahada ya sheria na baadaye akaanzisha kampuni ya filamu, katuni na vipindi vya ucheshi vya televisheni, Kvartal 95.
Kati ya miaka 2015-2019, Kvartal 95 ilirusha mfululizo wa vipindi vya televisheni vilivyoitwa Servant of the People ambapo Zelensky aliigiza kama Rais wa Ukraine.
Chama cha siasa Servant of the people kilianzishwa Machi 2018 na wafanyakazi wa Kvartal 95.
Tarehe 31 Desemba 2018, Zelensky alitangaza rasmi kuwa atagombea urais. Alifanikiwa kugombea na kushinda nafasi hiyo, na kwaka 2019 akaapishwa kuwa Rais wa Ukraine
Siku anaapishwa aliwaambia watunga sheria na wasomi. " Sitaki picha yangu ining'inie Ofisini kwenu, Rais sio Sanamu wala Mchoro, Wekeni picha za watoto wenu na muwe mnaziangalia kila wakati mnapofanya maamuzi"