RC Hapi Awachongea Wakuu wa idara kwa Rais Samia



MKUU wa Mkoa wa Mara (RC), Ally Hapi amemwomba Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kufumua wakuu wa idara mkoani humo wanakwamisha wakurugenzi kwani “wananuka rushwa.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Hapi amesema hayo leo Jumapili, tarehe 6 Februari 2022, mbele ya Rais Samia aliyetembelea ujenzi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Musoma mkoani Mara.

Amesema, tangu alipomteua kuwa mkuu wa mkoa huo, alikutana na changamoto katika halmashauri za Tarime Vijijini, Bunda na Musoma Vijijini ambako miradi ya maendeleo ilikuwa haifanyiki.

“Tarime walikuwa wanapewa fedha kutoka mgodini, fedha zinakwenda na miradi haifanyiki, Bunda kulikuwa na ujenzi wa makao makuu ya halmashauri, wazabuni wamelipwa zaidi ya Sh.400 lakini vifaa havikapelekwa sababu hawana pa kuziweka,” amesema.



“Mheshimiwa Rais, tunakushuruku ulituletea wakurugenzi wapya katika maeneo yote haya, lakini tuna wakuu wa idara ambao bado wako kwenye mfumo uleule wa upigaji,” amesema

RC Hapi amesema, “Mheshimiwa Rais bila kufumua…watu wa manunuzi, mipango, hawa Ma DMO wametengeneza urafiki na hawa wa manunuzi.”

“Mkurugenzi kila ukimwelekeza anakutana na hawa wakuu wa idara, ni walewale waliofisadi miradi ya maendeleo. Tumebadili wakurugenzi, wakuu wa wilaya lakini wakuu hawa wa idara wananuka rushwa, wana urasimu mkubwa na wanakumbatia ufisadi. Tunaoma utusaidie katika hili ili,” amesema Hapi huku wananchi wakishangiliwa


Naye Mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara amemwomba Rais Samia kufanyika kwa ukaguzi maalum hatika halmashauri kwani kuna ufisadi wa kutosha kwenye eneo hilo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad