Refa kawaonea Man U? Watmore mkono uligusa mpira, ufafanuzi wa kisheria



Man United leo wameondolewa katika michuano ya FA Cup na Middlesbrough baada ya dakika 120 za mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1, mikwaju ya penati Middlesbrough wakashinda 8-7.

Utata uliibuka dakika ya 64 Middlesbrough walipopata goli la kusawazisha kupitia kwa Crooks aliyepata assist safi kutoka kwa Watmore ambaye mkono wake ulianza kugusa mpira kabla ya kutoa assist lakini muamuzi aliruhusu kuwa goli.



Nimeona nikuaogezee vifungu vya sheria ya soka kutoka IFAB na uniachie maoni yako kwa sheria inayosema muamuzi alifanya maamuzi sahihi au alikosea?

Sheria namba 12 ya mchezo wa soka kwa mujibu wa Bodi ya chama cha kimataifa cha utungaji na usimamizi wa sheria za soka IFAB.



“Itatafsiriwa kuwa mchezaji ameshika mpira kwa mkono (hand ball) kwa kukusudia endapo mkono/kiganja chake kitakuwa hakipo katika eneo lake la asili wakati mkono ukigisa mpira, mkono umesaidia kumeongeza umbo la mwili”



Mkono wa mchezaji wa Middlesbrough aliyetoa assist na kuzaa goli la Middlesbrough haukuwa katika eneo lake la asili je muamuzi alifanya maamuzi sahihi?.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad