Ruto njiapanda sasa baada ya kupuuza vyama



Naibu Rais William Ruto aliharibu nafasi ya kushirikiana na vyama vidogo vya kisiasa na kujiweka katika hali hatari kisiasa, alipokuwa akivumisha chama cha United Democratic Alliance (UDA) kwa wapigakura.

Hatua hii imeanza kumsumbua huku viongozi wa vyama hivyo hasa vilivyo na mizizi eneo la Mlima Kenya wakimlaumu kwa ubaguzi.

Dkt Ruto alitawanya vyama vidogo ambavyo mwanzoni vilikuwa vikimuunga mkono alipojitenga na chama cha Jubilee.

Alipoungana na chama cha Amani National Congress (ANC) cha aliyekuwa makamu wa rais Musalia Mudavadi na Ford Kenya cha Seneta wa Bungoma Moses Wetang’ula, alichukuliwa kama aliyepoteza nafasi nyingine ya kufungulia milango vyama vidogo.


 
Aliyekuwa Gavana wa Kiambu William Kabogo, aliongoza chama chake cha Tujibebe Wakenya, kushirikiana kwa muda mfupi na muungano wa Kenya Kwanza, lakini anaonekana kujitoa huku akikosa kuhudhuria mikutano ya kisiasa ya Dkt Ruto, Mudavadi na Wetang’ula.

Mara kadhaa, Dkt Ruto amekuwa akipuuza na kudharau vyama vidogo akiviita vyama vya kijiji na kimaeneo vinavyofaa kuvunjwa au kukataliwa na wapigakura.

Hatua hii imefanya baadhi ya vyama vya kisiasa na waliokuwa washirika wake wa kisiasa kujipanga kivyao kabla ya uchaguzi mkuu ujao na kuyumbisha umaarufu wa Dkt Ruto mashinani kote nchini.


Rais Kenyatta ambaye ni kiongozi wa Jubilee naye anaonekana kutumia hatua hiyo kukusanya vyama vidogo kuunga azma ya aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga anayetaka amrithi baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Baadhi ya vyama hivyo ni Chama Cha Kazi (CCK) cha mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria na The Service Party cha aliyekuwa waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri, bado havijatangaza mwelekeo kuhusu muungano kabla ya uchaguzi mkuu ujao.Chama cha People’s Democratic Party (PDP), kinachoongozwa na Gavana wa Migori Okoth Obado pia kilishirikiana na UDA kwa muda mfupi.

Ni Chama cha Mashinani (CCM), kinachoongozwa na aliyekuwa Gavana wa Bomet Isaac Ruto, kinachoonekana kushirikiana na UDA licha ya kutokuwa na mkataba wa ushirikiano.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Nairobi Kipkirui Kemboi Kap Telwa, anasema kwamba, baadhi ya vyama vidogo viliundwa na washirika wa Rais Kenyatta kwa lengo la kugawanya umaarufu wa Dkt Ruto katika maeneo tofauti.

Anasema kwamba lengo la kuundwa kwa vyama hivi vidogo ilikuwa ni kupunguza uungwaji mkono wa Dkt Ruto katika maeneo tofauti.

“Raila hajakumbatia vyama vipya na iwapo atashinda urais chini ya muungano wa vyama vingi vya kisiasa, basi itakuwa vigumu kuendesha serikali. Maspika wanaweza kutoroka na bunge na pia kuzima bajeti za miradi na wizara muhimu,” alisema Bw Kap Telwa.

Alisema kwamba Naibu Rais alijivuta kukumbatia vyama vidogo vya kisiasa kwa sababu anajua hatari ya miungano ya kisiasa kama hiyo.

Wapinzani wafanya maombi ya pamoja
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad