Sakata la Mondi kutumia Bendera ya Ubaguzi, Wakazi, Sallam Wafikia Pabaya


LILE sakata la supastaa wa Bongo fleva, Diamond Platnumz kutumia bendera inayoashiria masuala ya ubaguzi wa rangi katika video yake ya GIDI limeibua sura mpya kufuatia rapa maarufu nchini, Wakazi kumjibu Meneja wa Diamond, Sallam Sk akidai kuwa huwa hajibishani na watu DM isipokuwa wale anaowadai na wawanawake anaowapenda na kuwaheshimu tu.

Hii imekuja baada ya Wakazi kumshauri Diamond aiondoe video hiyo kisha aihariri (editing) kisha aipandishe tena YouTube jambo ambalo lilimuibua Sallam na kumponda Wakazi akisema kuwa watu kama Wakazi wamekuwa wakimfuata DM wakiwa na shida zao lakini wakitaka kukosoa Biashara zake wanakwenda mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Wakazi amejibu tena na kusema; ”PISI KALI AU NAKUDAI ?! 🤷🏾‍♂️ Nyie mnaosema Sallam amenijibu kwa hiyo tweet, mngeenda kumuuliza awape jibu kabla ya kutoa taarifa sizizo na uhakiki.

Kwanza sidhani kama jamaa hana ujasiri wa kuni address moja kwa moja kama zamani. Pili siwezi kuwa mimi maana Privately I only talk to “women I adore” & People naowadai hela. Sikupigii unless ni vitu hivyo.

Sasa huyo boss wenu mnataka kusema anadaiwa na mimi au? maana sio pisi kali. Akiwaambia kweli alinilenga mimi basi jueni ni muongo… tuna mahusiano rafiki, lakini sio ya kupigiana simu kuombana misaada. Na last time i checked, he called me.

I got receipts as usual. Najua ni mambo ya uswahili kutaka kuaminisha watu uongo, maana niliona mswahili mwenzake Hamisi Taletale anajicommentisha… Kumbukeni kabla ya Chitown mimi ni mwanadaresalamu, na wakati mpo Mji Kasoro mi nilikuwa Stakishari na Wazaramu, kabla Wachagga na Wanyakyusa hawajapatawala.

Mdomo ninao. Y’all can formulate opinions, it is fine… BUT WE ARE CONTROLLING THE NARRATIVE! The Leader,” ameandika Wakazi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad