Sakata la Shaffih Dauda Kutokuwepo Katika List ya Mawakala wa Michezo Mwenyewe Afunguka "Sijawahi Kuwa Wakala"


Nimeiona barua kutoka TFF kuhusu Mawakala wanaotambulika na chombo hicho kinachoendesha mpira wetu nchini, maswali yamekuwa mengi kwa Wadau kuwa kwanini sipo kwenye orodha hiyo

Niseme tu kuwa sio kosa la TFF na Mimi sijawahi kuwa wakala na sijawahi kuwa na leseni bali Kampuni yangu ya SHADAKA ilikuwa na Wakala wake anayewakilisha taasisi, Ibrahim Mohamed, ambaye baada ya miaka miwili hakurenew tena leseni yake

Hivyo ni sahihi wao kutoitambua @shadakasports hilo halina tatizo, ni fair kwa pande zote mbili, kwanini Ibrahim wa SHADAKA hakurenew leseni? Pengine labda ndio swali ambalo wengi mnajiuliza, pengine mnajiuliza nafanyaje shughuli za kimpira?

Well, tulifanya research yetu nzuri tu kuhusu soka letu nchini na vipaji vyetu kwenye soko la Kimataifa, nikaona kwa nilipofikia napaswa kufanya INTERNATIONALIZATION OF TALENTS, yani nichukue vipaji hivi kuvipeleka duniani kwenye maisha makubwa zaidi kimpira

Dauda hafikirii kufanya biashara ya ndani ya wachezaji, hafikirii kuhamisha Mchezaji kutoka labda Ndanda kwenda Simba, Kagera kwenda Yanga bali anafikiria kumchukua Mchezaji kutoka Mbao akacheze Abu Dhabi, kutoka Biashara akacheze Israel, ndio project ya @shadakasports

Kwa kutambua project hii, sikuona sababu ya kuwa na leseni ya ndani, sikuona pia sababu ya kuwa na leseni ya uwakala kwakuwa nimeamua kufanya Joint venture, nafanya kazi na Kampuni kubwa za Uwakala duniani

Naweza kutumiwa recommendation kutoka Tel Aviv, Abu Dhabi au Lisbon, Cairo ama Casablanca kuwa wanahitaji Mchezaji fulani mwenye quality fulani kazi yangu ni kuwatafutia aina hiyo, kupitia agencies kubwa ambazo nafanya nao kazi, hapo sikuona sababu ya leseni

Nikikwambia kuna baadhi ya Wachezaji wazawa wanashea Agency na MO SALAH utanielewa?? Well simple ndio maana nikasema nafikiria zaidi soko la kimataifa la Vijana wetu, kazi yangu kuwafikisha pale, hii haihusiani na Uwakala bali jicho la kuona potential na kuisogeza kwa Top Agencies kisha waingie kwenye top teams, with top payments

Mpaka sasa tumepush transfers 10 za Kimataifa, Said Jr (Baniyas), Salamba (JS Saoura), Mpepo (Interclub), Kyombo (Mamelodi), Mafie (Abu Dhabi), Tibar John (Abu Dhabi) mifano tu

When DIGALA speaks you listen

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad