Serikali imefuta Ibara ya 24 iliyokuwa inapendekeza kifungu kipya 47A kwa lengo la kutoa Mamlaka kwa Polisi kufanya operesheni za kificho kwa madhumuni ya kuzuia utendaji wa makosa
Taarifa iliyotolewa Bungeni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Eliezer Feleshi imesema katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai uliopitishwa jana, kifungu hicho tata kimeondolewa rasmi
Muswada huo uliopelekwa Bungeni kwa hati ya dharura uliibua sintofahamu kwenye mitandao ya kijamii huku Wananchi wakihoji mantiki ya kuwakingia kifua Askari Polisi endapo watafanya jinai na kuhalalisha mauaji ya raia