Serikali Yaelekeza Kushusha Bei ya Vifaa vya Ujenzi Vilivyopandishwa Kiholela



Serikali imesema tathmini iliyofanyika imebaini ongezeko holela la bei ya vifaa vya ujenzi hususan saruji na nondo linasababishwa na wazalishaji wa bidhaa husika kufanya uzalishaji banifu

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Ashatu Kijaji amesema wamebaini ongezeko limesababishwa na kutokuwa na mfumo wa wazi wa usambazaji wa bidhaa kutoka kiwandani mpaka kumfikia mlaji wa mwisho

Ameelekeza Wazalishaji na Wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi kushusha mara moja bei za bidhaa walizopandisha kiholela. Mamlaka za Udhibiti zimeagizwa kuchukua hatua dhidi ya walimbikizaji na wauzaji kupitia mlango wa nyuma (black market) wanaosababisha bei za bidhaa kupanda sokoni


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad