Shaffih Dauda Atoa ya Moyoni Malalamiko ya Yanga "Tusifanye Kisa Yanga na Simba, Tufanye Kwa Mpira"




Asubuhi nilisema kitu kuhusu Yanga na press yao kuhusu Waamuzi, mitazamo ilikuwa tofauti na majibu yalikuwa ni mengi, ni kawaida yangu kusoma maoni na kujua wapi nikazie tena

Kwenye mpira wetu huu kama penati ya utata kati ya Namungo na Yanga sio stori, kama uamuzi wa utata kati ya Simba na Mtibwa labda sio stori, bali stori ni offside ya Mayele dhidi ya City basi kuna shida sehemu

Imetokea mitazamo mingi ikiwemo ujio wa VAR, lakini shida yetu ya msingi ni hawa Waamuzi ambao ndio wataziendesha hizo mashine, kama Mwamuzi hawezi kukubali bao la Namungo mbele ya Simba, bao la Kagera mbele ya Yanga ndie ataendesha VAR?

Kama Mwamuzi ambaye bado hajui tafsiri sahihi ya offside au faulo kisha ndie huyu akaendeshe VAR?? Tunachohitaji ni uthubutu kwanza kisha teknolojia, tunahitaji reformation kwanza kisha teknolojia

Bado tuna safari ya kuwekeza kwenye rasilimali watu, yes Professional investment kwanza kama ambavyo duniani wamefanya kisha usaidizi wa teknolojia, kama hujui formular hivi unaweza kutumia scientific calculator?

Wanazuoni wanasema Development ni gradual ni hatua kwa hatua! Je tuna hivyo viwanja bora?? Vipo vingapi?? Je tuna vingapi vina system nzuri ya umeme?? Tuna Wataalam wangapi wenye uwezo wa kutafsiri kwa usahihi??

Bado tuna matatizo mengi kabla ya kwenda huko, nje na hapo tunapiga mark time tu! Kabla ya kuziwaza Simba na Yanga tuuwaze kwanza mpira wetu, kabla ya kuwaza hawa wawili kwanza tupambane kuipackage ligi yetu

Tunachofanya ni kutengeneza sumu mbaya, kuzipa ukiwa timu nyingine zinazoitwa ndogo, kwamba ikiwa vibaya kwa Mbeya City au Dodoma Jiji sio stori, ila stori ni miamba pekee??

Bado nafikiri kupambana kwenye upatikanaji wa waamuzi, malipo ya waamuzi na utoaji wa kozi kwa Waamuzi, bado vita ya kutaka chama huru cha Waamuzi kisha twende huko

Bado tufahamu Waamuzi wanalipwa vipi, wanaendesha vipi maisha yao kuelekea mechi, ni binadamu hawa, tuna mengi ya kumuomba Mungu kabla ya kumuomba utajiri

Ndio tunataka kuruka ila tuagane na nyonga! Elimu ianze, uchumi ufuate kisha Teknolojia ifate

DIGALA WAS HERE
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad