WAKATI msanii wa Bongo Movies, Rose Alphonce almaarufu Muna Love akimrudia Mungu wake na kumuomba toba kwa kile alichokifanya huku akienda mbali zaidi kwa kuwasihi watu wasifanye sajari, hatimaye shepu hizo bandia, zinazidi kutikisa Bongo, .
Wiki kadhaa zilivuja tetesi kwamba mwanamama Aunt Ezekiel naye amekwea pipa kwenda nchini India kwa ajili ya kutengeneza shepu, lakini mwenyewe alikanusha kabla ya jana kukiri kufanya hivyo
Aunt ameshtua wengi baada ya ile shepu yake ya mwanzo kubadilika; yaani amekuwa na shepu matata mithili ya Beyonce wa Jay Z wa Marekani.
MUNA LOVE; Miongoni mwa watu ambao walikuwa mstari wa mbele kujinadi kuwa amefanya upasuaji wa viungo vingi kwenye mwili wake ikiwemo dimpozi, tumbo, shepu, midomo na sehemu nyingine, ni pamoja na mwanamama Muna Love.
ZARI THE BOSS LADY
Zari amejizolea umaarufu mkubwa nchini Tanzania baada ya kuzaa watoto wawili na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul almaarufu Diamond Platnumz.
TANASHA DONNA
Kama ilivyo kwa Zari, mwanamama Tanasha naye amepata umaarufu mkubwa baada ya kuzaa mtoto mmoja wa kiume na Diamond aitwaye Naseeb Junior. Miaka miwili iliyopita wakati akiwa Bongo kabla ya kurejea nchini kwao, Kenya, baadhi ya watu walionekana kumsema kuhusu shepu yake kuwa siyo matata, lakini naye mwaka jana alidaiwa kwenda kufanya sajari ya kutengeneza umbo lake na sasa ana umbo namba nane na kiunio cha nyigu
HAMISA MOBETO
Hamisa ndiye alikuwa mrembo wa kwanza Bongo kuamsha mastaa wenzake baada ya kudaiwa kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kufanya upasuaji na kutengeneza shepu.
POSHY QUEEN
Mwanamama Poshy Queen ndiye anatajwa kuwa tishio kutokana na umbo lake lilivyojigawa na kuwa na kiuno chembamba. Madai yaliyopo ni kwamba, kabla ya kufanya sajari umbo lake lilikuwa tofauti kabisa na alivyo sasa kwa ushahidi wa picha zake za zamani.
VERA SIDIKA
Hata hivyo, huwezi kuhitimisha listi hii bila kumtaja mwanamama maarufu Afrika Mashariki akitokea nchini Kenya, Vera Sidika kwani anatajwa kuwa ndiye ‘mwalimu’ wa wanawake wengi waliofanya sajari kwa kuwa wanamtazama alivyokuwa awali na sasa ana umbo namba nane na kuvutia wengi.