Sheria ya HABARI, Serikali Yasema Ipo Tayari Kupokea Mapendekezo



Akiulizwa ikiwa Vyombo vya Habari kufungiwa kutategemea Hisani ya Kiongozi mmoja hadi mwingine au upo utaratibu wa kuhakikisha vinafanya kazi kama taratibu zinavyoelekeza, Rais Samia amesema Vyombo vya Habari vitafanya kazi kwa Mujibu wa Sheria

Katika Mahojiano Maalum na DW, Rais Samia ameeleza, "Vyombo vikikiuka Sheria vinafungiwa, ndiyo maana Sheria ipo. Hakuna Nchi ambayo ina Vyombo vya Habari vinafanya vinavyotaka bila kufuata #Sheria"

Amesema Serikali ipo tayari kupokea Mapendekezo kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016, ambapo baadhi ya vipengele vimekuwa vikilalamikiwa kuwa kandamizi

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad