Mtoto wa muigizaji Yvonne Cherrie @soniamonalisa amejikuta akifunguka ya moyoni mara baada ya baadhi ya watu haswa kwenye mitandao ya kijamii kumdhihaki kwa kuchagua kwenda kusoma nchini Ukraine ambapo kwa sasa kuna vita kubwa.
Sonia ambae yupo Ukraine kupata masomo ya ngazi za juu, ameeleza kusikitishwa na baadhi ya watu wanao fanya mzaha na uwepo vita nchini Ukraine kwa kumdhihaki kuwa alikataa kusoma vyuo vy hapa nchini na sasa anapitia wakati mgumu katika nchi hiyo.