Spika wa Bunge Awaonya Mawaziri



SPIKA wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewataka mawaziri na manaibu wao kuhudhuria ipasavyo vikao vya Bunge kutokana na baadhi yao kusuasua kushiriki vikao hivyo.

Akizungumza juzi wakati wa kuahirisha shughuli za Bunge, Spika Tulia alisema: "Mnadhimu wa Serikali, mimi ninafahamu na ndiyo maana siku zote huwa ninasema hapa, hata mbunge akisema waziri simwoni, serikali ipo bungeni.

"Ni kweli serikali ipo bungeni lakini sote tunafahamu Waziri Mkuu ambaye ni mbunge lakini ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni lakini huwa anahudhuria bungeni na anakaa bungeni kusikiliza hoja za wabunge.

“Kama hakuonekana hapa, yupo kwenye kikao au amesafiri. Sasa wapo mawaziri, wapo Dodoma hayupo kwenye kikao lakini hayupo bungeni.

"Na pia wapo manaibu mawaziri wapo Dodoma, hawapo kwenye kikao lakini hayupo bungeni. Sasa tunakuwa tunalikosea heshima Bunge."


Dk. Tulia alisema wale ambao wapo kwenye kikao, Mnadhimu wa Serikali anatakiwa awe na taarifa nao.

“Kuna wale ambao hawapo kwenye kikao, hawajaitwa na Rais, Makamu wa Rais, wala Waziri Mkuu, wale ambao wanakuwa huko kote hawapo, wahakikishe wanakuwapo bungeni kwa sababu pamoja na kwamba wanapelekewa taarifa na utaratibu upo mzuri kabisa, ila lengo la serikali kuwa sehemu ya Bunge ni pamoja na wao kuwapo bungeni, wakati hoja za wabunge zikizungumzwa na wananchi ni vizuri mawaziri wakasikiliza wenyewe, ” alisema.

Aliomba suala hilo lisisitizwe kwenye vikao vyao ili kuhudhuria ipasavyo vikao vya Bunge.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad