Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema suala la anuani ya makazi zitakamilika kabla ya kuanza zoezi la uhesabu watu na makazi.
Amesema hayo katika kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambapo amesema hatua hiyo itasaidia katika kuhesabu watu.
“Suala la Anuani ya makazi liliombwa na Jaji Mkuu kwa kuwa linarahisisha kutoa huduma ya mahakama kwa wananchi,” amesema Rais Samia.