Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) imetoa Msaada wa Euro Milioni 425 (Tsh. Trilioni 1.15) kwa ajili ya kugharamia Miradi ya Maendeleo
Fedha zilizotolewa zinatarajiwa kutumika katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa miaka mitatu ijayo huku Serikali ikainisha kutumia Tsh. Bilioni 480 (Euro Milioni 180) kwenye miradi mitatu ikiwemo kuimarisha Mifumo ya Kidijitali
Aidha, Rais wa EC, Ursula von der Leyen amesema #Tanzania ni miongoni mwa Nchi za Afrika zitakazonufaika na mpango mpya wa EU (Global Gateway Investment Package) unaokusudia kukabiliana na changamoto ikiwemo Ajira na kuimarisha Huduma za #Afya na Elimu