Taratibu za Kuwaondoa Watanzania Ukraine Zinafanyika



Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki, imesema inaendelea kuchukuwa hatua za haraka kwa Watanzania walioko nchini Ukraine.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na mkurugenzi kitengo cha mawasiliano ya Serikali Emmanuel Buhohela, imeeleza kuwa watanzania hao takriban 300 waliopo nchini humo wataondolewa na kupelekwa nchi za Poland na Romania ambako kuna kuna utulivu na kuwawezesha kufika nchini kwa usalama.


Aidha Serikali imeweka wazi kuwa hakuna mtanzania aliyepata madhara kutokana na hali inayoendelea nchini humo.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad