MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema, inafuatilia wale wote ambao wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa maandishi ‘sms’ wa kuwashawishi watu kujiunga na Freemason. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Hayo yamesemwa leo Jumanne, tarehe 22 Februari 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabir Bakari katika kikao kati ya mamlaka hiyo na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
Dk. Bakari alikuwa akijibu swali la mmoja wa wahariri, aliyetaka kujua kama laini zote za simu zimesajiliwa, kwa nini hao wanaotuma ‘sms’ hizo hawachukuliwi hatua.
Akijibu kwa kifupi, Dk. Bakari amesema, “tuko kazini kwenye hilo tuacheni.”
Aidha, mkurugenzi huyo amesema, hadi kufikia Desemba 2021, laini zote za simu zimesajiliwa “kwa hiyo hakuna uhalifu unaoweza kufanyika tusimjue. Laini zote zimesajiliwa na kama kuna changamoto mbalimbali, tunazifanyia kazi