TFF Yawarudisha Waamuzi Wote Darasani



SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), jana Jumatano liliweka wazi kuwa limeandaa semina ya siku tatu kwa
waamuzi wote wa Ligi Kuu Bara kwa ajili ya kuwaandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.


Lengo kuu la semina hiyo ni kutazama, kupitia changamoto na kuboresha maeneo mbalimbali ili kuondoa zile sintofahamu za uamuzi Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo kwa malalamiko ya wadau mbalimbali wa soka juu ya changamoto za waamuzi kushindwa kuzitafsiri vema sheria za soka katika baadhi ya mechi za Ligi Kuu Bara zilizopita.

 

Katika malalamiko hayo, vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, Yanga walienda mbali zaidi na kuandaa
mkutano wa waandishi wa habari juzi Jumanne kuelezea masikitiko yao na mwenendo wa baadhi ya waamuzi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad