Kundi la wadukuzi linalojiita 'Yemen Hackers' limedai kudhibiti Tovuti 34 za Serikali ya Msumbiji na kutaka lipewe takriban Tsh. Milioni 46 (Dola za Marekani 20,000)
Wadukuzi wamesema wanataka Fedha hiyo ndani ya saa 24 au watavujisha taarifa za siri zikiwemo za Wizara ya Ulinzi. Fedha wanayoitaka itatakiwa kutumwa kwa Bitcoins. Serikali inatarajiwa kuzungumzia Udukuzi huo leo Februari 23, 2022