Tuache unafiki, Wasafi wapewe pongezi kubwa sana


Tuache unafiki, Wasafi wapewe pongezi kubwa sana.

Event ya mahaba Ndi Ndi Ndi wameiandaa vizuri sana.

Wamepiga promotion ya kutosha kiasi kwamba hakuna mtanzania ambaye hajui kwamba Tar 14 kuna tukio gani Dar es Salaam, aisee Wasafi ni kiboko mnoooo.

Watu walioalikwa katika event hiyo pia ni wa moto sana, nimeona kila status ipo pale kuna wasanii, wanasiasa, viongozi wa serikali, watu wa ulinzi na usalama n.k.

Wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuibrand event hii, kiasi kwamba kila mtu anatamani siku hiyo afike akiwa na  couple yake.

Nimewanyooshea mikono juu baada ya kuona kwamba Wasanii wa nyimbo za malavidavi Kassim mganga, Q chillah na wengine kibao wataperform siku hiyo, aisee huu ni unyama mkubwa mno, unaanzaje kukosa tukio kama hili? Kumbuka kwamba show hii ni mara moja kwa mwaka, haijirudii hii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad