Tukio la Kutisha Mauaji Kanisani..Amuua Mfanyakazi Mwenzake na Kuutenganisha Mwili na Kiwili Wili Kwa Panga




Polisi Mkoani Njombe wamemkamata Daniel Mwilango kwa tuhuma za mauaji ya Nickson Myamba (48) aliyekuwa Katibu wa Baraza la Walei Kanisa la Roman Katoliki Kigango cha Parokia ya Makambako yaliyotokea February 08, 2022, Mwilango amekamatwa Wilayani Mvomero, Morogoro.

RPC wa Njombe, Hamis Issa amesema Mtuhumiwa amekamatwa akiwa na vitu mbalimbali vya Marehemu "Simu ya Marehemu alikuwa anayo yeye pamoja na funguo ikiwemo ile ya chumba ambacho tukio lilitokea, Mtuhumiwa huyo amekiri na kuonesha vitu alivyotumia katika mauaji ikiwemo panga aliliokuwa amelitupa chooni, chuma alichotumia kumpiga Marehemu, ndoo na vitambaa vilivyotumika kwa ajili ya usafi wa damu kwenye chumba yalipotendekea mauaji"


"Mauaji yalitokea kwenye duka la vitabu lililopo katika eneo la Kanisa hilo ambapo Mtuhumiwa alijiandaa na kutumia chuma kizito kumpiga mwenzake kisogoni, alipopoteza fahamu alimuongezea chuma kingine na hili pigo la pili lilimsababishia Nickson Kufariki, alichokifanya Daniel alitumia panga kuutenganisha mwili, kiwiliwili, kichwa na kifua vilikuwa sehemu yake halafu na kiuno na miguu vilikuwa sehemu yake”


"Tunamshikilia pia Mlinzi wa Kanisa hilo anayeitwa Nickson Valentine kwa kushiriki katika tukio hilo, upelelezi unaendelea na hadi sasa tumebaini chanzo ni chuki za Mtuhumiwa dhidi ya Marehemu, ukimuuliza anasema 'Marehemu ni tishio la maisha yangu kwasababu amepewa kazi zangu' na anamuhisi Marehemu ndiye aliyesababisha yeye akaondolewa kwenye sehemu ya duka na miradi mingine wakati yeye aliondolewa kwasababu ya ubadhilifu na sio vinginevyo”
#MillardAyoUPDATES

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad