Tukio la Uporaji Kwenye Magari; Polisi Watoa Tamko



Siku kadhaa zilizopita, video ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwaonesha kundi la vibaka, wakiyavamia magari yaliyopo kwenye foleni na kufanya uporaji wa kutumia silaha.

Wapo waliodai kwamba tukio hilo limetokea katika Daraja la Salenda jijini Dar es Salaam, taarifa ambazo hazikuwa na ukweli.

Ukweli ni kwamba tukio hilo limetokea katika Barabara ya Broadhurst jijini Gaborone, Botswana na tayari Jeshi la Polisi nchini humo, limetoa taarifa kwa umma za kuwataka wasamaria wema, kulisaidia jeshi hilo kuwatambua wahalifu hao.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Botswana, Botswana Police Service, tukio hilo limetokea Februari 11, 2022 na kwamba jeshi hilo linaendelea na msako mkali huku likitoa namba za simu kwa yeyote atakayefanikisha kuwatambua wahalifu hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad