Tunasubiri Tupewe Sababu za Diamond Kutumia Confederate Flag Kwenye GIDI, Hawa Hapa ni Mastaa Waliowahi Kutumia na Wakatoa Ufafanuzi



Ishu ya Msanii Wakazi kumtaka Diamond kurekebisha sehemu ya video yake ya Gidi ambayo inamuonyesha yupo sehemu ambayo kuna bendera “Confederate Flag” ambayo ni ishara ya ubaguzi wa rangi huko nchini Marekani, imekuwa ni kubwa sana mitandaoni na kila mmoja akiongea lake.

Hawa ni mastaa wanne (4) wa Marekani ambao wamewahi tumia bendera hiyo hadharani na wakashambuliwa vikali lakini walikuwa na sababu zao.

2005, Rapa tokea Atlanta, Ludacris alivaa vazi lenye bendera hiyo kwenye performance yake katika tuzo za VIBE AWARDS na baada ya show akalivua vazi hilo na kubakiwa na vazi lenye rangi tatu,Nyeusi,kijani na Nyekundu. baadae akatolea ufafanuzi akidai alivaa vazi hilo kuwakumbusha watu kuwa ni wapi tulikotoka na vazi alilobakia nalo mwilini ni kuwaambia ni wapi tunakotaka kwenda maana ni rangi ya Afrika, Luda alisema bendera hiyo ina maana mbaya kwa jamii hasa watu weusi ambao waliteswa na kunyanyapaliwa vibaya sababu ya rangi yao, na ndio maana wimbo alioimba “Georgia” kwenye tuzo hizo una ujumbe wa racism.

Kanye West ni moja ya marapa waliowahi kutupia bendera hiyo, 2013 na akaiweka hadi kwenye bidhaa zake baada ya wimbo wake wa NEW SLAVE, Kanye alipofanya Interview na Los Angel radio 97.1AMP, alidai anajua kipindi cha nyuma walikuwa watumwa,lakini bado anaamini kuna ishara zote kuwa bado utumwa upo na ndio maana akajiita New Slave na kuitumia bendera hiyo.

Lil Jone alitumia bendera hizo kwenye Cover ya Albamu yake,lakini Ukitazama Bendera hizo zinawaka moto, Lengo lilikuwa kutokomeza ubaguzi kwa watu weusi ambao bado ulikuwa ukiendelea kwa jamii, nchini Marekani.

Andre 3000 alifananisha meseji ya wimbo wake wa Ms Jackson na kile kilichokuwa kikitokea enzi ubaguzi wa rangi.

Tunasubiri tupewe sababu za Diamond kutumia confederate Flag kwenye GIDI😁

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad