Rais wa Kenya anayekaribia kumaliza muda wake Uhuru Kenyatta kwa mara ya kwanza ametangaza kumuunga mkono rasmi Kiongozi wa Chama cha ODM Kenya Raila Odinga kuwa ndiye anafaa kuwa Rais wa Kenya kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Akihutubia mbele ya Wajumbe katika eneo la Mlima Kenya, Kenyatta ameitaka jamii yake kumuunga mkono Odinga akisema kwamba anaheshimu maslahi ya Taifa.
Kiongozi huyo bila kumtaja Naibu wake William Ruto ameonekana kumpiga dongo Ruto huku akisema hatokuwa na tatizo nae katika siku za usoni iwapo atabadilika "Nawaomba mumuunge mkono Raila Odinga kwasababu anapigania maslahi ya Taifa hili, Kijana wangu atakapobadilika tutamfikiria pia nae"
Hii ni mara ya kwanza Rais Uhuru Kenyatta ameiambia jamii yake hadharani kwamba anatamani Mrithi wake awe Raila Odinga japo kwa siku zote amekuwa akimuunga mkono Odinga bila kumtaja moja kwa moja.