Ukraine ilipovamiwa Kininja



KWA Siku mbili mfululizo miji mbalimbali ya Ukraine, imekuwa sawa na tanuri la moto baada ya wanajeshi wa Urusi, kushambulia kila upande kwa kutumia anga, ardhini na majini.

Haijajulikana rasmi athari iliyotekea katika mashambulizi makali yanayoendelea, lakini ni wazi watu wengi watakufa, majengo yatabomolewa na miundombinu mbalimbali inatekezwa kwa mabomu.

Vita hiyo kati ya Urusi na Ukraine imekuja baada ya miezi kadhaa ya vita vya maneno kati ya nchi za Magharibi ikiongozwa na Marekani na Urusi, huku Rais Vladimir Putin, akikanusha angevamia jirani yake.

Hata hivyo, asubuhi ya Alhamisi hali ilibadilika ghafla baada ya uvamizi kuanza kwa mashambulizi makali ya mabomu kutoka katika ndege vita na manoari za kijeshi zilizotia nanga baharini.

Kutokana na uvamizi huo, sasa Putin anashutumiwa kwa kuvunja amani ndani ya bara la Ulaya, na endapo vita hiyo ikizidi kushika kasi ni wazi usalama wa bara hilo utakuwa mashakani.


Majeshi ya Urusi wameshambulia kutoka wapi?

Katika mashambuzili ya siku ya pili, viwanja vya ndege na makao makuu ya jeshi vilipigwa mabomu. Karibu na miji yote nchini Ukraine inashambuliwa na uwanja mkuu wa ndege wa kimataifa wa Boryspil katika mji mkuu wan chi hiyo Kyiv, nao unazidi kuharibiwa kwa mabomu.

Wakati mashambuliz ya anga yanashika kasi, vifaru na wanajeshi wa ardhini wamengia Ukrainia kaskazini-mashariki, karibu na Kharkiv, jiji lenye watu milioni 1.4, ambao uko mashariki karibu na Luhansk kutoka nchi jirani ya Belarusi.


Wanajeshi walikamata kambi muhimu ya anga nje kidogo ya Kyiv, na wanajeshi wa Urusi walitua katika miji mikubwa ya bandari ya Odesa na Mariupol.

Kabla ya kuanza uvamizi huo, Rais Putin alitangazia dunia kupitia runinga kwamba Urusi haiwezi kujisikia salama, kuendeleza na kuwepo kwa sababu ya kile alichokiita tishio la mara kwa mara kutoka kwa Ukraine ya kisasa.

Hoja zake zililenga kuwalinda watu wanaodhulumiwa na mauaji ya halaiki na pia kuondoa utawala wa kinazi ndani ya Ukraine. Hata hivyo Rais wa Ukraine, Volodymr Zelensky, anakana kwamba ana siasa na Nazi, pia anafananisha mashambulizi yanayofanyika ni sawa na uvamizi wa Ujerumani ya Nazi katika Vita vya Pili vya Dunia.

Rais Putin mara kwa mara amekuwa akiishutumu Ukraine kwa kuchukuliwa na watu wenye itikadi kali, tangu kiongozi wake anayeiunga mkono Urusi, Viktor Yanukovych, kuondolewa madarakani mwaka 2014.


 
Urusi kwa muda mrefu imekuwa ikipinga hatua ya Ukraine kutaka kujiunga na Umoja wa Ulaya na muungano wa kijeshi wa kujihami wa nchi za Magharibi Nato. Inaishutumu Nato kwa kutishia mustakabali wa taifa hilo kiusalama.

NGUVU ZA KIJESHI

Inakadiriwa idadi ya wanajeshi wa Urusi walioingia ndani na wanaokaribia Ukraine inaweza kuwa kati ya 100,000 na 190,000.

Ijumaa iliyopita, Marekani ilisema Urusi imetuma wanajeshi kati ya 169,000 na 190,000.

Michael Carpenter, balozi wa Marekani katika Shirika la Usalama na Ushirikiano la Ulaya (OSCE), anasema Idadi hiyo inajumuisha wanajeshi walioko karibu na mpaka na Ukraine, na Belarus, na Crimea ambayo ilichukuliwa miaka ya nyuma.


Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace, anasema asilimia 60 ya wanajeshi wa Urusi wanatola Belarusi.

Kwa upande mwingine, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine, ametoa idadi ya wanajeshi 149,000.

Hata hivyo, Urusi haijasema chochote kuhusu idadi ya wanajeshi wake.

Lakini Jumuiya ya kujihami ya NATO ilisema kwamba haijaona ushahidi wowote wa hii ardhini.
Wanasema kuwa theluthi mbili ya jeshi liko ndani ya kilomita 50 kutoka mpakani.

Picha za satelaiti pia zinaonyesha kuwa baadhi ya wanajeshi wa Urusi wamegawanywa katika vikundi vidogo ambao wameingia Ukraine kwa urahisi.


 
Uwezo wa kijeshi wa Ukraine

Jeshi la Ukraine ni dogo zaidi kuliko lile la Urusi, lakini linapata usaidizi kutoka kwa Jumuiya ya Kujihami ya Nchi za Magharibi NATO.

Marekani haijatuma wanajeshi humo, lakini imetuma wanajeshi 3,000 zaidi nchini Poland na Romania ili kuimarisha vikosi vya NATO, na imewaweka wanajeshi wengine 8,500 katika hali ya tahadhari.

Marekani pia imetuma silaha zenye thamani ya dola milioni 200, ikiwa ni pamoja na kombora la kushambulia vifaru la Javelin na kombora la kudungua ndege la Stinger. Pia imeruhusu nchi wanachama wa NATO kukabidhi silaha zilizotengenezwa Marekani kwa Ukraine.

Uingereza imepeleka makombora 2,000 ya kushambulia vifaru ya masafa mafupi nchini Ukraine, imetuma wanajeshi 350 zaidi nchini Poland, na kuongeza mara mbili uwezo wake wa kijeshi kwa kutuma wanajeshi 900 zaidi nchini Estonia.

Uingereza imetuma ndege zaidi za kivita kusini mwa Ulaya na meli ya wanamaji pamoja na wanajeshi wengine wa NATO kupiga doria bahari ya Mediterania.

Pia imewatahadharisha wanajeshi wake 1,000 ili iwapo kutatokea shambulio, wasaidie wakati wa mzozo wa kibinadamu nchini Ukraine.

Denmark, Uhispania, Ufaransa na Uholanzi pia zimetuma wanajeshi na meli zao Ulaya Mashariki na mashariki mwa Mediterania.

Urusi itakwenda mbali na lengo?

Urusi imekataa kusema kama inataka kupindua serikali iliyochaguliwa kidemokrasia ya Ukraine, ingawa inaamini kwamba nchi hiyo inapaswa kusafishwa kutoka kwa Wanazi. Rais Putin alizungumzia kuwafikisha mahakamani wale waliofanya uhalifu mwingi wa umwagaji damu dhidi ya raia.

Kwa kutambua maeneo yanayoungwa mkono na Urusi yaliyojitenga ya Luhansk na Donetsk kama huru, alikuwa tayari ameamua kuwa hayakuwa tena sehemu ya Ukraini.

Jamuhuri za watu wanaojiita huru zinachukua zaidi ya theluthi moja ya maeneo yote ya Luhansk ya Ukraine na Donetsk lakini waasi wanatamani mengine pia.

Uvamizi unahatarisha vipi Ulaya?

Vita hiyo ni jambo la kutisha kwa watu wa bara zima la Ulaya, wakihuhudia urusi ikivamia nchi jirani ya Ulaya kwa mara ya kwanza tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Makumi ya watu wamekufa tayari katika kile Ujerumani imekiita Vita vya Putin.

Viongozi wa Ulaya wamelaani na umeleta saa za giza zaidi tangu miaka ya 1940.

Emmanuel Macron wa Ufaransa, anasema uvamizi huo unaonyesha kunatakiwa hatua ya mabadiliko katika historia ya Ulaya.

Ofisa mkuu wa jeshi la Marekani, Mark Milley anasema ukubwa wa vikosi vya Urusi unamaanisha hali ya kutisha katika maeneo yenye miji mikubwa.

Uvamizi huo una madhara makubwa kwa nchi nyingine nyingi zinazopakana na Urusi na Ukraine, kama Latvia, Poland na Moldova.

Hali ya hatari imetangazwa nchini Lithuania na Moldova, ambako maelfu ya wanawake na watoto tayari wameingia kama wakimbizi.

Nchi za Ulaya zaiacha Ukraine

Nchi za Ulaya zimeonekana kujitenga katika viya hiyo na kubakia kuiwekea vikwazo Urusi na kuiacha serikali ya Ukraine ikipigana peke yake.

Hata hivyo, Nato imeweka ndege za kivita katika hali ya tahadhari, lakini muungano huo umeweka wazi hakuna mipango ya kutuma wanajeshi wa kivita ndani ya Ukraine. Badala yake wametoa washauri, silaha na hospitali za kutumiwa vitani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad