Juhudi za kumuokoa mtoto nchini Morocco ambaye alianguka katika kisima karibu na mji wa Chefchauone zinaelekea ukingoni
Mtoto huyo , ambaye vyombo vya Habari vya eneo hilo vimemtambua kuwa wa miaka mitano , Rayan , alidaiwa kucheza karibu na kisima hicho katika mji wa kaskazini wa Tamrout , yapata kilomita 100 kutoka mji wa Chefchaouen.
Rayan anaaminika kuanguka mita 32 kupitia mwanya mdogo wa shimo hilo. Operesheni ya uokoaji ikiongozwa na idara ya kuwalinda raia , imekuwa ikiendelea tangu siku ya Jumanne.
Uokoaji wa mtoto huo unakaribia, msemaji wa serikali Mustapha Baitas alisema siku ya Alhamisi jioni.
''Mioyo yetu ipo na famÃlia na tunaomba kwamba atajiunga não hivi karibuni’’.
Licha ya kuanguka vibaya, picha zilizoingizwa katika kisima hicho zinaonesha kwamba mvulana huyo bado yuko hai na ana fahamu, licha ya kwamba anaonekana kujeruhiwa kichwani.
Wafanyakazi wa uokoaji wameshusha maski ya hewa , chakula na maji ndani ya kisima hicho na kikosi cha matibabu pia kipo katika eneo hilo, tayari kusaidia na kumtibu mtoto.
Ndege aina ya helikopta pia imewasili katika eneo hilo ili kumpeleka hospitali punde tu atakapookolewa kutoka kwa kisima.
Maelfu ya watu wamekuwa wakitazama picha za uokoaji huo kutoka kwa mitandao ya kijamii , na kundi kubwa la watazamaji limekongamana katika eneo hilo.