Uongozi wa Mtibwa Sugar, umebainisha kuwa, Februari 23, kikosi chao kipo tayari kuvunja rekodi ya Yanga ya kutopoteza mchezo hata mmoja kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, ambapo Mtibwa watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye Uwanja wa Manungu, Morogoro.
Ikumbukwe kuwa, Mtibwa Sugar wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo kwa mabao 3-1 pamoja na kutolewa hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Coastal Union kwa kipigo cha 2-0 mbele ya Coastal Union.
Akizungumza na Spoti Xtra, Afisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema wanafahamu kwamba mchezo dhidi ya Yanga utakuwa wa mwisho kumaliza mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara, hivyo kutokana na nafasi mbaya waliyopo kwenye msimamo, lazima wahakikishe wanapata ushindi