Urusi imepiga marufuku ndege zote zenye uhusiano na Uingereza kupitia anga yake.
Haya yanajiri baada ya Uingereza kusitisha meli ya shirika la ndege la Urusi Aeroflot kugusa chini Uingereza, ili kukabiliana na uvamizi wa Ukraine.
"Marufuku ya matumizi ya anga ya Urusi umewekwa dhidi ya safari za ndege zinazomilikiwa, zilizokodishwa au kuendeshwa na shirika linalohusishwa au kusajiliwa naUingereza," mamlaka ya anga ya Urusi ilisema.
Ilielezea uamuzi huo kama jibu la "maamuzi yasiyo rafiki ya mamlaka ya anga ya Uingereza"