Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya uwepo wa Kimbunga Batsirai katika maeneo ya Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi. Kimbunga hicho kilijitokeza Januari 27, 2022 na kimesogea Kisiwa cha #Madagascar
Mamlaka hiyo imesema uchambuzi wa Mifumo ya Hali ya Hewa unaonesha kutokuwepo kwa uwezekano wa Kimbunga hicho cha Batsirai kufika katika Pwani ya #Tanzania
Maeneo yanayotarajiwa kupata vipindi vya Mvua kubwa kutokana na uwepo wa Kimbunga hicho ni Mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na Rukwa.