Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa akizungumza katika hotuba yake kwa njia ya video, akisema majeshi ya nchi yake yamesitisha mpango wa Urusi wa kumkamata usiku wa kuamkia leo na kumweka kiongozi wao wenyewe.
Pia aliwataka Warusi kumshinikiza Rais Vladimir Putin kusitisha uvamizi huo. "Tumeharibu mpango wao," Zelensky alisema.
Vikosi vya Ukraine vilikuwa vinadhibiti Kyiv na miji mikuu inayoizunguka, alisema.
Wakati huo huo Meya wa Jiji la Kyiv Vitali Klitschko ametangaza amri ya kutotoka nje katika jiji hilo kuu la Ukraine kati ya saa kumi na moja jioni na sasaa mbili asubuhii majira ya Ulaya (15:00-06:00 GMT).
Amri hiyo inayoanza kutekelezwa leo, rinabatilisha amri ya awali ya kutotoka nje kati ya saa nne usiku na saa moja asubuhi .
Akiandika kwenye Twitter, Klitschko alionya: "Raia wote watakaopatikana mitaani wakati wa kafyu watachukuliwa kuwa washirika wa hujuma za adui na makundi ya upelelezi."