Uvamizi wa Ukraine wamuweka matatani bilionea wa Chelsea


Wakati mataifa yakiendelea kulaani kitendo cha Russia kuivamia Ukraine, hali inazidi kuwa ngumu kwa bilionea Roman Abramovich baada ya hoja ya kutaka avuliwe umiliki wa Chelsea.

Chelsea ni moja ya klabu kubwa na zenye mafanikio barani Ulaya, hadhi iliyoipata baada ya kuanza kumilikiwa na raia huyo wa Russia, tovuti ya Fortune imeripoti.

Abramovich, ambaye alijivunia mabilioni ya dola kutokana na biashara ya mafuta na ambaye anaripotiwa kuwa mtu wa karibu wa rais wa Russia, Vladimir Putin, aliinunua klabu hiyo ya London mwaka 2003.

Tangu awekeze klabuni hapo, Chelsea imetwaa mataji 18 makubwa, yakiwemo mawili ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.


 
Gazeti la The Times liliripoti mapema mwezi huu kuwa mali nyingi za Uingereza zenye thamani ya pauni 1.5 bilioni zilinunuliwa na raia wa Russia ambao wana uhusiano na serikali yao, huku karibu mali za thamani ya pauni milioni 430 zikiwa katikati ya London.

Wakosoaji wamelipachika suala hilo jina la "Londongrad."

Jana majeshi ya Russia yalivamia Ukraine, huku serikali ikisema wataendelea kuunga mkono waasi wa nchi hiyo na majeshi hayataondoka hadi waone "matokeo".


Wakati suala hilo likiendelea kutikisa dunia, utajiri wa Abramovich unaanza kuangaliwa kwa makini zaidi pamoja na uhusiano wake wa karibu na Putin.

Mbunge wa chama cha Labour, Chris Bryant ndiye anayeongoza kampeni hiyo bungeni, akitaka Abramovich aondolewe katika umiliki wa Chelsea.

Jana alisema wakati wa maswali ya biashara bungeni kuwa aliziona nyaraka za kuanzia mwaka 2019 zikimuhusisha Abramovich na "shughuli chafu", imeandika tovuti ya Fortune.

Mwaka 2021, Abramovich alimshtaki mwandishi wa vitabu, Catherine Belton kwa kuandika katika


 
kitabu chake cha "Putin's People" kuwa Abramovich alifanya shughuli nyingi za kibiashara "kwa maelekezo ya Putin", ukiwemo ununuzi wa Chelsea. Baadaye shauri hilo lilimalizwa.

Chris Bryant ameishauri serikali ya Waziri Mkuu Boris Johnson kutaifisha mali za Abramovich za nchini Uingereza, ikiwemo klabu ya Chelsea na kampuni yake ya uwekezaji ya Millhouse LLC, imeripoti BBC.

"Kwa kweli, Abramovich hatakiwi kuendelea kumiliki klabu katika nchi hii? Hakika, tunatakiwa tuangalie kutaifisha mali zake ... na kuhakikisha kuwa watu wengine wenye visa ya daraja la kwanza kama huyi hawahusiki katika shughuli chafu," Bryant aliliambia gazeti la

The Guardian.Tangu mwaka 1994, wakati Russia ikifungua uchumi hali kadhalika China, wawekezaji wa


kigeni walikuwa na uwezo wa kununua ukazi wa Uingereza kwa kutumia programu ya "golden visa".

Lakini mpango huo ulisitishwa wiki iliyopita, wakati Puting alipozidisha tishio dhidi ya Ukraine, ikiwa ni baada ya kutuhumiwa kuendesha shambulizi la kemikali za neva kusini mwa jiji la Salisbury.Mmoja wa wanufaika wa mpango huo ni Abramovich.

Jumanne iliyopita, Boris Johnson alisema tayari Abramovich alikuwa anakabiliwa na vikwazo, lakini baadaye serikali ikakanusha.

Tayari Uingereza imeshaweka vikwazo kwa benki za Russia na matajiri wake.

Utajiri wa mafuta wa Abramovich umekuwa ukichunguzwa kwa miaka kadhaa na mwaka 2018, aliondoa maombi yake ya visa ya mwekezaji baada ya shutuma kuwa kubwa. Amekuwa akitumia hati ya kusafiria ya Israel kuingia Uingereza na hata wakati fulani kuishi kwenye boti zake za kifahari baada ya kukataliwa kuingia Uingereza.


 
UEFA yaipokonya Russia fainali Ligi ya Mabingwa

Paris itakuwa mwenyeji wa fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka huu baada ya jiji la Saint Petersburg kupokonywa mechi hiyo kutokana na Russia kuivamia Ukraine, Chama cha Soka Ulaya (UEFA) kimetangaza leo. Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad